Programu ya likizo ya Desemba kwa watoto wenye mahitaji maalumu
Usiache mtoto mwenye mahitaji maalumu akae bila mazoezi, usimwache nyumbani akitembea tembea tu..!!!! Likizo ya shule mara nyingi ni wakati mzuri - kwa watoto na familia kuwa pamoja baada kipindi kirefu cha masomo.
Hata hivyo, kwa familia zenye watoto wenye mahitaji maalum hasa mtoto mwenye usonji, likizo ya shule inaweza kuwa wakati mgumu. Sarm’s Occupational Therapy and Rehabilitation Centre imepanga program maalum katika likizo hii ya Desemba. Programu hii imekusudia kuwazoeza watoto katika maeneo yafuatayo:
- Uwezo wa kuwasiliana
(Ikiwa mtoto wako anapata shida kuzungumza lugha, hatua muhimu ni kuimarisha uwezo wake wa kuwasiliana) - Uwezo wa kutumia akili vizuri.
(kujipangilia, kutulia na kuwa makini, Kufanya kazi na kuimaliza nk) - Uwezo wa kuchangamana na watoto wengine.
(kufanya kazi kwa vikundi, kushirikiana na watoto wengine, kuomba msaada nk)
Program hii pia hutoa fursa nyingi za kucheza, za kuwasiliana zilizoandaliwa kwa ajili ya watoto walio na mahitaji maalum kuanzia umri wa miaka 2 hadi 9 kuwa mchangamfu. Wazazi wenye watoto wenye mahitaji maalum, wana fursa ya kuwaandikisha watoto wao kwenye programu hii. Usiache mtoto mwenye mahitaji maalumu akae nyumbani akitembea tembea tu.
Kwa habari zaidi, tafadhali zungumza na Mratibu wa Programu ya Likizo kwa kupiga namba 0656050300 au 0784 056682.
December-Holiday-Program-sw [155 KB]
Your Comments / Reviews
© Copyright 2024 Sarm’s Occupational Therapy and Rehabilitation Centre